Nafasi za Kazi Serikalini 2026: Matangazo Mapya

Nafasi za Kazi Serikalini 2026: Matangazo Mapya


Serikali ya Tanzania kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inaendelea kutoa fursa mbalimbali za ajira kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika katika kada za afya, elimu na kada nyinginezo. Kupitia SwahiliJobs.com, tumekuletea kiunganishi kitakachokuwezesha kupata matangazo mapya ya nafasi za kazi serikalini, kutambua nafasi zilizotangazwa hivi karibuni na kuwasilisha maombi yako kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal.

Ili kuomba nafasi hizi, waombaji wanatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa Ajira Portal na kujaza taarifa zao kwa usahihi. Katika hatua ya usajili, utahitaji namba ya NIDA ambayo utaitumia kuthibitisha utambulisho wako baada ya kuamilisha akaunti kupitia barua pepe. Baada ya hapo, utaendelea kujaza taarifa binafsi, mawasiliano na taarifa za kitaaluma.

Katika sehemu ya taarifa za elimu, unatakiwa kuthibitisha namba zako za mtihani wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kupitia mfumo. Kwa mfumo huu, taarifa hizo zinathibitishwa mtandaoni bila kuhitaji kupakia vyeti vya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Pia, waombaji wenye elimu ya chuo wanapaswa kujaza taarifa za chuo walichosoma, mwaka wa kuanza na kumaliza masomo pamoja na GPA, kisha kupakia vyeti vya elimu na transcript zinazohitajika.

Ni muhimu kuhakikisha vyeti vya chuo, transcript, CV na cheti cha kuzaliwa vinaandaliwa kulingana na masharti ya mfumo. Nyaraka zinazohitajika kuthibitishwa na mwanasheria zinapaswa kuwa na muhuri wa mwanasheria anayetambulika kabla ya kuskaniwa na kupakiwa kwenye akaunti yako. Pia, utatakiwa kujaza kiwango chako cha uwezo wa kutumia lugha ya Kiingereza katika kuzungumza, kusikiliza na kuandika, pamoja na kupakia picha yako ya passport size.

Baada ya kukamilisha taarifa zote, hakikisha unazihakiki na kuthibitisha kuwa ni sahihi kabla ya kutafuta nafasi za kazi na kutuma maombi kupitia akaunti yako. Waombaji wanashauriwa kufuata masharti yote yanayoonekana kwenye mfumo wa Ajira Portal ili kuepuka makosa yanayoweza kuathiri maombi yao.

Angalia Matangazo Mapya ya Ajira Serikalini 2026

Kupitia kiunganishi kilichoandaliwa na SwahiliJobs.com, unaweza kufuatilia matangazo ya nafasi za kazi yanayotolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Chagua tangazo linaloendana na elimu na sifa zako, soma masharti yake kwa makini na tuma maombi kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal.

Baada ya kutuma maombi, endelea kufuatilia akaunti yako kwa taarifa za hatua zinazofuata, ikiwemo kuitwa kwenye usaili. Ukipata mwaliko wa usaili, hakikisha unafuata maelekezo ya tangazo na kwenda na vyeti halisi (original certificates) pamoja na nyaraka nyingine zitakazohitajika.

Tembelea swahiliJobs.com mara kwa mara ili kupata matangazo mapya ya ajira serikalini, taarifa za usaili na fursa nyingine za kazi nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments